The House of Favourite Newspapers

TCRA Yavipiga Faini Baadhi ya Vyombo vya Habari

0

MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) Julai 1, 2020 imevitoza faini ya takribani shilingi milioni 30 vituo vya televisheni sita na kutoa onyo pamoja na kusitishiwa kwa muda uchapishaji wa maudhui.

Kituo cha Clouds Redio wamekutwa na kosa la maudhui ya kuhamasisha ngono kwa utumiaji wa supu ya pweza na wamepigwa adhabu Sh. milion tano na onyo kali.

Kituo cha DUMATV

Kosa:  Maudhui ya unyanyasaji kijinsia
Adhabu: Faini Sh. milioni saba na kufungiwa kwa muda wa mwezi mmoja

Kituo cha East Afrika Redio
Kosa: Kukashifu utendaji wa serikali katika uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya.
Adhabu: Sh. milioni tatu na onyo kali

SIBUKA TV
Kosa: Maudhui ya kushabikia mauaji
Adhabu: Tsh Milioni 3 na onyo

STAR TV
Kosa: Kukashifu viongozi wa Wilaya ya Kisarawe
Adhabu: Tsh Milioni 5 na waombe radhi siku tatu

Vituo vingine vilivyopigwa faini ni Global TV,  Ayo TV,  Abood Radio,  EFM Radio, Mo Radio, Clouds TV na Planet Radio

Leave A Reply