The House of Favourite Newspapers

Tecno Dude Ndiyo Simu ya Kijanja Mjini

0
Mdau akipozi baada ya kununua Tenco Dude

 

Katika kuadhimisha kilele cha Sikukuu ya Sabasaba, Kampuni ya Simu ya Tecno jana Ijumaa iliendelea na promosheni yake kabambe ya kuitangaza simu yao mpya ya Tecno Wx3 (TECNO DUDE) ambapo wananchi mbalimbali waliofika kwenye Maonyesho ya Sabasaba walionesha kushangazwa na uwezo wa simu hiyo ikilinganishwa na bei yake.

 

Mrembo akionesha Tenco Dude yake mpya

 

 

Simu hiyo ya aina yake inapatikana kwa bei nafuu ya Tsh. 180,000/= lakini ina kamera mbili pamoja na flash, kioo chenye sensor na sifa nyingine kibao kama zilivyoorodheshwa hapa chini:

  • Internet GSM/WCDMA
  • Android 7.o
  • Processor yake ni 1.3ghz Quad core
  • Ukubwa wa kioo inchi 5.0 Fwvga Touchscreen
  • Uwezo wa kamera ya nyuma ni 5mp na 5mp mbele pamoja na flash
  • 8GB Rom and 1GB Ram, micro sd inaongezwa hadi 32gb
  • 2500 mag battery
  • Connectivity Gps, Wifi, BT
  • Sensor G- Sensor

 

Tenco Dude kila kona.

 

Tecno ambao ni wadhamini wa Promosheni ya Bahati nasibu ya Shinda Nyumba ya Global Publishers, wamekuwa mahiri kwa kushusha simu kali na za kisasa ambazo pia ni za bei nafuu hivyo kuwafanya watumiaji wa simu kupendelea kutumia Tecno mara kwa mara ikilinganishwa na simu zingine.

 

Wahudumu wa Tecno wakimkabidhi mwanadada Tecno Dude yake baada ya kununua.

 

Picha hizi zinawaonyesha wadau na wapenzi wa SmartPhone wakiwa wenye tabasamu zito baada ya kila mmoja wao kununua TECNO DUDE mpya na kupata kuzifahamu faida na raha ya TECNO DUDE.

 

Leave A Reply