The House of Favourite Newspapers

TECNO KUJUMUIKA NA MASHABIKI KWENYE UZINDUZI WA SPARK 5PRO.

0


Kampuni ya simu TECNO yazindua rasmi TECNO Spark 5pro. Uzinduzi wa simu hiyo umefanyika Kidimbwi
Beach tarehe 18/10/2020 na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo komediani maarufu Jaymond
na wadau wa simu za TECNO.


Uzinduzi wa Spark 5pro ulifanyika katika mfumo wa party ambapo DJ Maphorissa kutoka South alitoa
burudani ya kutosha na kuufanya uzinduzi wa Spark 5pro kuwa wa aina yake.

“Spark 5pro sio simu ya kwanza kwa kampuni ya TECNO kuzinduliwa kwa mfumo wa party na hii
imejirudia kwasababu Spark 5pro ni simu yenye kutulenga vijana wa kileo na ili kuweza kutufikia kwa
uharaka zaidi basi ni lazima kutumia njia zetu kama hivi,

Baadhi ya sifa zinazopatikana katika simu hii ya TECNO spark 5pro ni uwezo wa simu hii kuwa na ukubwa
wa memory ya GB 64ROM + GB 3RAM, selfie ya megapixel 8 na kamera ya nyuma ni megapixel
16M+2M+2M+AI Lens, battery ya ujazo wa mAh 5000, alisema msanii maarufu wa comedian Jaymond
ambaye ndio mgeni mualikwa katika uzinduzi huo”.

“Uzinduzi wa Spark 5pro ni wa aina yake sisi kama wateja wa simu za TECNO tumefurahi kuona namna
TECNO inavyotujali na kututhamini, tumekula tumekunywa lakini pia tumepata nafasi yakupiga picha na
mgeni mualikwa alisema Bwana Haji Omary”.

TECNO Spark 5pro sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania.
Ili kufahamu mengi zaidi tembelea mara kwa mara ukurasa wa Instagram https://bit.ly/2Hftrh6

Leave A Reply