The House of Favourite Newspapers

TFF Watambua Mchango Wa Tahliso

Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Oscar Milambo amesema shirikisho hilo linatambua mchango wa Umoja wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso).

“Shirikisho linatambua mchango wa vyuo vikuu katika kukuza michezo nchini, hasa mpira wa miguu.

“TFF itaendelea kutoa mchango wao katika kuhakikisha michezo inaendelea vyuoni. Pia Mawaziri wa Michezo wa Tahliso walifikirie njia mbadala ya kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo Vyuo Vikuu Tanzania, Sophia Nchimbi amesema kuwa vikao vinavyojumuisha mawaziri wa michezo wa vyuo vikuu nchini, ni muhimu kufanyika mara kwa mara kwa lengo la kujadili na kukuza michezo vyuoni.

Naye Robert Manyerere ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) amesema shirikisho lao limefurahi kwa mualiko walipatiwa na kushauri ushiriki wa wanawake katika michezo.

Kwa upande wao Makamishna wa Idara ya Michezo na Burudani Tahliso, Hilary Urassa na Abdulrahim Khamis, walisema lengo la kikao hicho ni kukuza uhusiano kati ya mawaziri wote wa michezo wa vyuo nchini na kuwakutanisha pamoja kwa lengo la kukuza na kuendeleza michezo vyuoni.

Wamesema kuwa idara yao, imejikita katika kuinua michezo na burudani ifahamike nchini.

Nao washiriki wa kikao hicho, wameishukuru Tahliso kwa kuandaa kikao hicho na kusema wana imani kikao hicho kitazalisha mabadiliko katika sekta ya michezo vyuoni.

Nao wadau wa michezo nchini, wameshauri mawaziri hao kuangalia na michezo mengine na siyo mpira wa miguu pekee.

Na Neema Adrian.

Comments are closed.