TFF Yalaani Kauli ya Waziri Bashe

Shirikisho la Soka nchini TFF limesikitishwa na kauli ya Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, alioitoa baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi Jumamosi (Julai 03) kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans.

 

TFF imetoa taarifa ya kusikitishwa na kauli ya kiongozi huo, jana Jumapili jioni. Katika kurasa za mitandao za Waziri Bashe aliandika kuwa, “Waamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya Young Africans walidhibitiwa kwa makuaudi, vinginevyo wangetoa Penati”.

 

Katika taarifa hiyo TFF imewaomba viongozi wa kuacha hisia zinazoweza kuchochea vurugu kwenye mpira wa miguu, na badala yake wahubiri amani.

 

Katika mchezo huo Simba SC ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans, bao likifungwa na kiungo Zawadi Mauya.

 

Ushindi huo umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 70 zinazoiweka timu hiyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Simba SC yenye alama 73 inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu, na Julai 07 itacheza dhidi ya KMC FC jijini Dar es salaam.

4234
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment