The House of Favourite Newspapers

THEA, MIKE SANGU MAHABA BADO YAPO

MASTAA wa filamu za Kibongo, Mike Sangu na Salome Urassa ambao walikuwa ni mume na mke kabla ya kutengana kwa muda mrefu, juzikati walionesha kuwa bado wanapendana kwa kui­tana majina matamu, kitu ambacho kiliwaacha wengi mido­mo wazi.

Tukio hilo li­liloshuhudiwa na Ijumaa Wikienda, lilichukua nafasi maeneo ya Yombo Dovya jijini Dar ambapo wasanii hao walikwenda kutoa msaada kwa Hamisi, mtoto anayesumbuliwa na uvimbe.

Ilikuwa hivi; wakiwa eneo hilo mmoja wa wasanii alimtania Thea na kumwambia kuwa, Mike anamuita. Bila ku­tarajia Thea alimsogelea Mike na kumuuliza kwa sauti iliyotokea puani; ‘Eti kweli unaniita mume wangu?’

Maneno hayo yaliyotoka kwa sauti ya kimahaba yaliwafanya wasa­nii waliokuwa eneo hilo kuamini kuwa bado wawili hao wanapendana na huenda siku moja wakarudiana kwani waswahili wanasema; penzi la kweli halifi.

STORI: Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda

Watoto Waliowashinda WEMA na GABO Kwenye Tuzo Wafunguka “HATUKUTEGEMEA”

Comments are closed.