The House of Favourite Newspapers

Makambo Akikataa Kiatu cha dhahabu

Heritier Makambo raia wa DRC Congo

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo raia wa DRC Congo amesema malengo yake ni kuona Yanga inakuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na si yeye kuwa mfungaji bora na kuondoka na kiatu cha dhahabu kama wengi wanavyodhani.

 

Makambo ambaye kwa sasa ana mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara sawa na Salim Aiyee wa Mwadui, juzi Jumatano alikuwa mmoja wa wafungaji katika ushindi walioupata wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

 

“Kwa sasa malengo yangu ni kufunga mabao yatakayoiwezesha Yanga kupata pointi tatu na siyo kuwania kiatu cha ufungaji bora.

 

Timu yetu kwa msimu huu tumejipanga kutwaa ubingwa na siyo kuchukua tuzo binafsi. “Nataka kuona naendelea kufunga ili timu yangu iwe bingwa na wala sina malengo ya kuwa mfungaji bora, lakini kama ikitokea hivyo nitafurahi,” alisema Makambo.

Comments are closed.