The House of Favourite Newspapers

Tigo wazindua malipo ya kielekroniki Serikalini Arusha

Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha jana kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi akizungumza na wanahabari. 
Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka (kushoto)akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi muda mfupi kabla ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG).

 

 

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwasa) wamezindua mfumo mpya wa malipo ya kielekroniki serikalini (GePG) katika mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.

 

Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa Ankara mbalimbali pamoja na kufanya malipo kutokana na huduma wanazopata kutoka taasisi za serikali  zaidi ya 300 lengo ikiwa ni kurahisisha watumiaji wa huduma kutokaa katika misururu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo , Mkurugenzi wa Tigo  Kanda ya Kaskazini Nancy Bagaka alisema kuwa mfumo huo utapunguza kwa kiwango kikubwa ubadhirifu jambo ambalo litaongeza mapato ya serikali.

 

“Kutokana na mfumo huu faida nyingi zitapatikana ikiwemo kuongeza mapato ya serikali kupitia taasisi na mashirika , kuboresha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu , utoaji taarifa za mara kwa mara pamoja na kuondoa ubadhirifu na wizi” alisema Bagaka.

 

Aidha alisema ili kuweza kulipia Ankara mteja wa Tigo atatakiwa kupiga *150* 01# kisha atachagua kulipia ankra ambapo eneo la malipo ya serikali itajitokeza na kuingiza tarakimu 12  kwa taasisi anayotaka ipokee malipo.

 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Auwasa Edes Mushi alisema kutokana na mfumo huo mpya sasa wateja wa Mamlaka hiyo hawatolazimika kukaa katika misururu mirefu wakisubiri kulipia Ankara za maji.

 

“Auwasa kwa kushirikiana na Tigo tunaendelea kurahisisha maisha ya wateja wetu kwa kutumia mfumo huu wa GePG ambao tayari taasisi na mashirika mengi yanautumia”.

 

“Mbali na Auwasa, tayari Wizara ya Ardhi na Maenedeleo ya Makazi wanatumia, Shirika na Ndege ATCL , Bodi ya Utalii , Hospitali zote za umma , Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Wizara ya Mifugo nk .”

 

“Matumizi ya mfumo huu wa kielektroniki umerahisha utoaji huduma kwa wananchi na umeleta tija kubwa na kuongeza mapato hivyo tunasisitiza wateja wa Tigo wautumie ikiwa ni pamoja na kuulizia ankara zao za malipo ya maji” alisisitiza Mushi.

 

Mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watumiaji milioni 7 wa huduma ya Tigo pesa wanafanya malipo kwa haraka bila usumbufu kwenda kwa wakala ,idara na taasisi kadha wa kadhaa za Serikali.

Comments are closed.