The House of Favourite Newspapers

Tigo Yawapa Washindi 50 Tiketi za Kwenda Qatar Wengine Wajizolea Vifaa vya Hisense

0
Afisa Mkuu wa Tigo Pesa hapa nchini, Angelica Pesha (kushoto) akimpa Simon Meena mfano wa tiketi ya kwenda Qatar kujionea laivu michuano ya kombe la dunia.

 

 

18 Novemba 2022: SAFARI ya kwenda Qatar kuangalia kombe la dunia yaiva. Hayo yalisemwa na Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi zao washindi wa kampeni ya Wakishua Twenzetu Qatar ambapo idadi ya washindi 50 walikuwa wamekamilika.

 

Droo hizo zilianza kuchezeshwa awali na hii ya mwisho kupatikana washindi 8 ambao wanakamilisha idadi ya washindi 50 waliokuwa wakihitajika wa tiketi za kuingia uwanjani kushuhudia laivu kumbe la dunia. Akiwatangaza washindi hao mbele ya wanahabari Meneja Mary alisema droo ya mwisho ilifanyika Jumatano iliyopita na kuwapata washindi hao 8.

Afisa Masoko wa Kampuni ya Hisense, Joseph Mavura (kulia) akimpongeza Mariam Abdi Kassim wakati akimkabidhi vifaa vya Hisense vinavyoonekana nyuma yao vikiwa kwenye maboksi yake. Kushoto Ni Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta.

 

 

Meneja Mary amesema pamoja na washindi hao 50 kuhitimisha zoezi la washindi wa tiketi mchongo huo utaendelea kwa kugawa vifaa vya nyumbani vya Hisense na kuwataka wateja wa Tigo kuendelea kutumia huduma za Tigo Pesa kufanya miamala na kuweza kuibuka washindi kwa droo zinazoendelea.

 

“Safari ya washindi wetu itakuwa katika makundi matano ambapo kundi la kwanza litaanza kuondoka Novemba 29 na kundi la mwisho Desemba 5.

Afisa Mkuu wa Tigo Pesa hapa nchini, Angelica Pesha akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukabidhi tiketi za kwenda Qatar kushuhudia laivu michuano ya kombe la dunia.

 

 

“Safari hiyo itaanzia hapa nchini kupitia Dubai ambapo wakifika hapo watapumzika na kuangalia manzari ya mji huo na kisha waanza tena safari ya kuelekea Qatar na wakati wa kurudi pia watapitia tena Dubai kuangalia tena manzari ya mji wa Dubai na ndiyo watarudi hapa nchini” alimaliza kusema Meneja Mary.

 

Kwa upande Afisa Masoko wa Hisense, Joseph Mavura amesema pamoja na kuhitimisha zoezi la utoaji wa tiketi za kwenda Qatar kampeni hiyo itaendelea kwa kutoa vifaa vya nyumbani vya Hisense ambavyo ni pamoja na Tv za nchi 50 ambazo ni za kisasa HD4K, Friji la ujazo wa lita 120, Micro Wave yenye ujazo wa lita 30 pamoja na muziki wa kisasa (Sound Bar).

 

Mavura ameendelea kusema kuwa sambamba na kuendelea kampeni hiyo maduka yote yanayouza vifaa vya Hisense hapa nchini yataendelea kutoa punguzo la asilimia 20 bidhaa zake na mteja atafikishiwa bidhaa yake mpaka kwake.

 

Kwa upande Afisa Mkuu wa Tigo Pesa hapa nchini, Angelica Pesha aliyefika kwenye tukio hilo kwa ajili ya kukabidhi tiketi ya kwenda Qatar kwa mshindi aliyekuwa akifunga dimba alisema anafuraha kubwa sana kuwa na wateja wake hao walioshiriki kampeni hiyo kwa kufanya miamala ya Tigo Pesa.

 

Afisa huyo baada ya kumkabidhi tiketi mshindi huyo aliyefunga dimba aliwaomba watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa tigo na kutumia huduma za Tigo Pesa ili kuweza kuibuka vifaa vya Hisense katika mchongo huo unaoendelea. Alimaliza kusema Angelica.

Leave A Reply