Timu Tano Zamfuata Kagere Simba

WAKALAwa mchezaji Meddie Kagere wa Simba, Patrick Gakumba, amesema kuwa amepokea ofa tano za mteja wake huyo na kama hataendelea kupata nafasi ya kucheza ndani ya timu hiyo, basi itabidi ahame mara baada ya kumaliza mkataba wake.

 

Kagere amekuwa akikosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza katika michezo miwili mfululizo ya ligi, huku kocha wa Simba Sven Vandenbroeck akionekana kumtumia zaidi mshambuliaji John Bocco.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Gakumba alisema kuwa mteja wake huyo amebakisha mkataba wa mwaka mmoja hivyo kama ataendelea kutopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza itabidi aondoke ndani ya Simba kwani amepokea ofa nyingi.

“Kagere kuhusu kutocheza ndani ya Simba ni jambo ambalo hapendezwi nalo na mimi kama mteja wake sipendi kumuona mfungaji bora wa Ligi ya Rwanda na Ligi ya Tanzania mara mbili mfululizo akiwekwa benchi, hivyo tutaangalia nini cha kufanya mara baada ya mkataba wake kumalizika.

 

“Mpaka sasa nina ofa zaidi ya tano za Kagere, timu nyingi zimekuwa zikimhitaji lakini nashindwa kufanya mazungumzo nao kwa kuwa Kagere bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia Simba, ila ukifika muda wa kuanza kufanya mazungumzo kila kitu kitakuwa hadharani,” alisema wakala huyo.

Stori: Marco Mzumbe,Dar es Salaam

Toa comment