The House of Favourite Newspapers

Tishio La Corona Lampa Hofu Baba Samatta

0
Mzee Ally Samatta

BABA mzazi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta amesema kuwa amekuwa na hofu kubwa juu ya mtoto wake kutokana na kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa Covid19 unaosambazwa na kirusi cha Corona katika nchi za Ulaya kufuatia baadhi ya mechi kuchezwa bila ya mashabiki.

 

Kesho Jumamosi, Samatta anatarajiwa kuiongoza Aston Villa kucheza dhidi ya Chelsea katika mchezo Ligi Kuu England utakaopigwa kwenye Uwanja wa Villa Park huku timu hiyo ikiwa katika mapambano ya kujinasua kushuka daraja kutokana na kuwa na pointi 25 katika nafasi ya 19.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, mzee Samatta alisema kuwa suala la kuwepo kwa ugonjwa wa Covid19 duniani limekuwa likimpa presha kubwa kutokana na mtoto wake kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaocheza kwenye ligi kubwa.

“Kiukweli suala la huu ugonjwa sina raha nao hasa kutokana na mtoto wangu kuwepo Uingereza na juzi hapa kuna mechi imesitishwa kwa sababu ya ugonjwa huo ambao unaenea kwa kasi kubwa duniani.

 

“Uzuri nimeongea naye na hata nilivyokuwa kule nimemsisitiza juu ya suala la kutokupenda kwenda kwenye mikusanyiko ambayo haina ulazima,” alisema mzee Samatta.

Stori Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Leave A Reply