The House of Favourite Newspapers

Tiwa Savage awashangaza mashabiki kwa kuvaa gauni la gunia

0

Tiwa-Savage-headies-600x600Mwanamuziki machachari wa Nigeria, Tiwa Savage.

MWANAMUZIKI machachari wa Nigeria, Tiwa Savage, majuzi aliwashangaza mashabiki wake kwa kuvaa gauni la gunia kwenye hafla ya fasheni ya kampuni ya prodyuza ya Marvin Records.

image (4)….Akiwa amevaa gunia.

Bila kujali macho na maneno ya watu, nyota huyo mwenye mtoto mmoja alitinga katika hafla hiyo iliyokwenda kwa jina la One Lagos Concert iliyofanyika eneo la Ikorodu akiwa ‘ng’aring’ari’ katika gauni lililoshonwa kutokana na vipande vya magunia.

Katika ukurasa wake wa Instragram amekuwa akiwauliza mashabiki wake iwapo wanakubaliana au kupinga gauni hilo, majibu yao yamekuwa ni mengi mno – ya wale wanaokubaliana na kivazi hicho na wale wanaokipinga.

Leave A Reply