The House of Favourite Newspapers

Tizi La Simba Uturuki Usipime… Sadio, Kanoute ni Balaa!

0

BAADA ya Simba SC kutua Uturuki kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24, timu hiyo imeanza matizi chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Ikumbukwe kwamba, Julai 12, mwaka huu, Simba ilielekea Uturuki na kuanza mazoezi ikiwa na wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2022/23.

Miongoni mwa mastaa waliopo kwenye kikosi hicho ni Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, David Kameta, John Bocco na Henock Inonga.

Program ya Robertinho raia wa Brazil kwa siku ya kwanza ilikuwa kurejesha miili ya wachezaji katika uimara wao pamoja na mazoezi ya umiliki wa mpira.

Mbali na hilo, pia alikuwa akiwaandaa viungo kwenye kutengeneza mashambulizi na kufunga.

Program nyingine ambazo zinaendelea ni pamoja na gym kwa wachezaji wote kuimarisha misuli pamoja na kuwa fiti pamoja na mazoezi ya kujiweka sawa wakiwa kwenye bwawa la kuogelea.

Kwa upande wa makipa, nao walikuwa wakipewa mbinu na kocha mpya Daniel Cadena ambaye msimu wa 2022/23 alikuwa anawanoa makipa wa Azam FC.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA 

MZIGO wa JEZI za SIMBA WAONESHWA LAIVU KUZINDULIWA MLIMA wa KILIMANJARO, ONANA AITEKA SHOO

Leave A Reply