The House of Favourite Newspapers

Tone Records Yamuunga Mkono DC Kinondoni kwa Shindano la Uswazi Star Search

0

SAMSUNG CSC

Mratibu wa shindano hilo, Fredy Njeje akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

SAMSUNG CSC

Prodyuza mkuu wa Studio za Tone Records, Hassan Rajab ‘Hasa B’ akizungumzia shindano hilo.

SAMSUNG CSC

Mtunzi wa nyimbo za wasanii, Eddie Nyota akitoa mchango wake.

SAMSUNG CSC

Adili Chapakazi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

SAMSUNG CSC

Mwakilishi wa wasanii wa muziki, Hilder Magesa akizungumzia shindano hilo.

SAMSUNG CSC

Muonekano wa studio za Tone Records kwa ndani.

Stori: Denis Mtima
STUDIO ya Tone Records yenye makazi yake Mwenge jijini Dar, imeungana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi katika kuhakikisha wanainua vipaji vya vijana wa wilaya hiyo wenye uwezo wa kuimba kwa kuzindua shindano lililopewa jina la Uswazi Star Search.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Fredy Njeje alisema kuwa shindano hilo limejikita kwa njia ya mtandao ambapo mshiriki anatakiwa kutuma kipande cha video yake aliyojirekodi akiimba, kisichozidi dakika moja kupitia Mtandao wa Kijamii wa Whatsapp kupitia namba 0653 146 563 sambamba na kukiposti kipande hicho kwenye akaunti yake ya Instagram bila kusahau kuweka hanstag ya #uswazistarsearch.

Mratibu huyo alisema kuwa mshindi atapatikana kwa kushindanisha ‘likes’ ambapo mwenye likes nyingi kwenye video aliyoituma mtandaoni ndiye atapata nafasi ya kurekodiwa wimbo wake bure kabisa na kupewa promo ya wimbo huo.

Naye msanii mkongwe Adili Chapakazi aliyekuwepo katika uzunduzi huo amewataka wasanii wachanga kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa kipaji ni mtaji na wengi wametoka kupitia muziki.
Picha/ Denis Mtima

Leave A Reply