The House of Favourite Newspapers

Top 5: Wasanii Wenye Mkwanja Afrika

0

MUZIKI kama zilivyo biashara nyingine, unalipa. Kwa hapa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiye anayetajwa kuwa na utajiri mkubwa japo vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa wapo wasanii wenye uwezo kifedha zaidi yake lakini kimsingi Kibongobongo bado imekuwa ni vigumu sana kupata data halisi za utajiri, tofauti na mataifa ya wenzetu.

 

Hii ndio Top Five ya wasanii wenye pesa zao Afrika kwa mujibu wa majarida mbalimbali yanayofanya tathimini za utajiri ikiwemo Forbes Africa.

 

AKON

Huyu ndiye anayetajwa kuwa namba moja kwa utajiri Afrika. Ana utajiri wa dola milioni 80 (zaidi ya Bilioni 184.8). Mkali huyu ambaye jina lake kamili ni Aliaume Damala Badara Thiam, ni Mmarekani mwenye asili ya Senegal anayefanya muziki wa Hip Hop. Ana vipaji vingi, ni mwandishi wa mashairi, anaimba, mfanyabiashara, mzalishaji wa muziki na pia muigizaji. Anatajwa kuwekeza pia kwenye miradi mbalimbali iliyo tofauti na muziki.

 

BLACK COFFE

Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Nkosinathi Maphumulo, ni Msauzi ambaye anakamata nafasi ya pili kwa wasanii wenye mkwanja mrefu Afrika. Yeye ana utajiri wa dola milioni 60 (zaidi ya Bilioni 134.6). Ametokea KwaZulu-Natal, lakini amekulia katika Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini.

 

DAVIDO

Mwamba huyu kutoka Nigeria, mara kadhaa amekuwa akilinganishwa na baadhi ya watu Bongo kwamba levo zake zinafanana na Diamond, lakini namba zinaongea. Jamaa kimkwanja yuko vizuri kwani ameingia kwenye Tano Bora.

 

Davido ambaye jina lake kamili ni David Adedeji Adeleke, anakadiriwa kuwa na utajiri usiopungua Dola Milioni 16 (zaidi ya Bilioni 36.9).

 

DON JAZZY

Huyu ni mkali mwingine kutoka Nigeria. Naye anaingia kwenye Top Five, kwani anatajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 10 (zaidi ya Bilioni 23.1). Utajiri wake amewekeza kwenye kuzalisha muziki, kuandika na kupafomu nyimbo pamoja na ujasiriamali.

 

BANKY W

Jamaa huyu ambaye kimuonekano anatajwa kuwa bishoo, ndiye anayekamilisha orodha hii ya Top Five akitajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 9 (zaidi ya shilingi Bilioni 20. 7) Ni bosi wa E.M.E Record Laber ambaye mbali na muziki, amejikita kwenye biashara ikiwemo ya mawasiliano na Uber.

MAKALA | Erick Evarist

Leave A Reply