The House of Favourite Newspapers

Toto, JKT Ruvu Wacha Zishushane Daraja

0
Wachezaji wa Toto wakiwania mpira na wachezaji wa Toto.

Mwandishi Wetu | Championi Jumamosi | Habari

TOTO African na JKT Ruvu, zote zipo katika hatari ya kushuka daraja na leo zinakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Toto ikiwa mwenyeji.

JKT Ruvu ipo mkiani mwa timu 16 ikiwa na pointi 23 katika mechi 27 huku Toto ikiwa nafasi ya 14 na pointi 26 katika mechi 26. Majimaji ni ya 15 ikiwa na pointi 26. Kocha wa Toto, Fulgence Novatus, aliliambia Championi Jumamosi kuwa; “Tunataka kushinda mechi hii, kwani tukipoteza tutakuwa mahali pabaya na tunaweza kushuka na hatutaki iwe hivyo.

 

” Azish Kondo yeye ni Kocha Msaidizi wa JKT Ruvu, akizungumzia mchezo huo, alisema: “Haijalishi tupo katika nafasi gani, lakini tunachotaka ni ushindi ili tusishuke daraja na hatutaangalia Toto wapo katika hali gani.

” Kwa vyovyote vile, sare itaziweka pabaya zaidi timu hizo lakini yeyote atakayefungwa atakuwa amejiwekea njia ya kushuka daraja, hasa JKT Ruvu ambayo ikifungwa tu inashuka daraja.

Majimaji ambayo pia ipo katika hatari ya kushuka daraja, nayo leo Jumamosi inacheza na Mwadui FC nyumbani kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Ruvuma.

Wakati huohuo mshambuliaji wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Aprili kwa msimu wa 2016/17, akiwashinda Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City.

Leave A Reply