The House of Favourite Newspapers

TRA Wazipiga Pini Ofisi za TFF Kisa Madeni

Rais wa TFF Jamal Malinzi Akizungumza na vyombo vya Habari
Uwanja wa Karume zilizopo Ofisi za TFF
Jengo la Ofisi ya TFF

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepata pigo la aina yake baada ya kufungiwa kwa ofisi zake zilizopo Karume, Dar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na deni kubwa la kodi wanalodaiwa.
Ofisi hizo zimefungwa leo mchana chini ya Kampuni ya Udalali na Minada ya Yono, ambayo kwa sasa ndiyo inazishikilia ofisi hizo baada ya kuwatoa nje wafanyakazi wote wa TFF na kuwataka waache kila kitu ndani.
Hakuna Ofisa wa TRA aliyekuwa tayari kuzungumza haraka wakati wa zoezi hilo leo mchana, lakini habari zinasema ni madeni ya tangu uongozi uliopita, chini ya rais,Leodegar Tenga kabla ya uongozi wa sasa, chini ya Rais Jamal Malinzi.
Deni wanalodaiwa na TFF na TRA linatokana na kodi za mishahara ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazil Maximo kwa miaka minne tangu 2006 hadi 2010.
Deni lingine linalosababisha ofisi za TFF kufungwa ni la kodi ya Ongezeko la Thamani (VaT) la ziara ya timu ya taifa ya Brazil nchini mwaka 2010 ilipokuwa njiani kwenye Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alipotafutwa Rais wa TFF, Jamal⁠ Malinzi alisema; “Ni kweli nasikia hilo limetokea kwa sababu ya madeni ya kodi za mishahara ya ⁠⁠⁠Maximo na VaT ya mechi ya Brazil,”.
Malinzi akaongeza kwamba kutokana na tatizo hilo, msafara wa Tanzania uliokuwa unaelekea kwenye mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Afrika(Caf ) sasa upo Addis Ababa,ukisubiri kuunganisha ndege kesho urudi Tanzania.
“Msafara wa Tanzania uko Addis Ababa na kesho ni uchaguzi mkuu CAF na pia itapigwa kura ya Zanzibar kupewa uanachama wa CAF na Tenga kuingia FIFA, msafara inaabidi urudi na kuacha yote haya,”amesema Malinzi.

Kutokana na kufungwa kwa ofisi hizo kuna kila dalili mazoezi kwa imu ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys yakasimama kutokana na kuutumia Uwanja wa Karume, ulio ndani ya ofisi hizo.

Comments are closed.