TRACY AMENIPA FURAHA YA MOYO WANGU !

Mambo vipi mpenzi msomaji wa safu hii uipendayo ya staa na familia? kama ilivyo kawaida kazi yake ni kuwafikia mastaa mbalimbali na kujua maisha yao wanayoishi kila siku na familia zao. Leo ndani ya safu hii tunaye mwanamama ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga almaarufu Linah. Linah amejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Tracy ambaye amezaa na jamaa maarufu kwa jina la Director Ghost.

Kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda, Linah anafunguka jinsi anavyomlea mwanaye Tracy ambaye ndiye furaha ya moyo wake; ijumaa Wikienda: Linah wewe ni mama wa mtoto mmoja wa kike, je, unamlea peke yako au unasaidiana na baba yake? linah: Kama wazazi, wote tuna jukumu la kumlea mtoto wetu. Haijalishi kama tupo pamoja au hatupo pamoja. ijumaa Wikienda:

Vipi kuhusu baba wa mtoto, huwa anamtembelea au kumchukua kukaa naye kwa sababu inajulikana kuwa hamuishi pamoja? linah: Unajua mimi huyu mtoto sijamzaa peke yangu ni wa kwetu mimi na baba yake. Kwa hiyo siwezi kumzuia kumchukua mtoto na pia mwanangu anapata mapenzi ya baba na mama. Kuhusu kuishi wote, hilo siwezi kulizungumzia kwa kuwa

mara nyingi mwanamke anazaa kwa ajili yake haijalishi baba anamsaidia au laa. ijumaa Wikienda: Unapenda nini kutoka kwa mtoto wako? linah: Huwa napenda alivyo mchangamfu, anapenda kucheka na mara nyingi huwa napenda kucheza naye.

Huwa ninajisikia sina amani siku akiumwa hivyo ninajitahidi kumuwaisha kwa daktari wake ili aweze kuwa sawa na tuendelee na furaha kwani ndiye furaha ya moyo wangu. ijumaa Wikienda: Ukitoka kwenda kwenye shoo nje ya nchi au hata hapahapa nchini, lakini mbali na nyumbani huwa unajisikiaje? linah: Huwa ninajisikia mpweke, lakini kwa kuwa huwa nina uhakika nimemuacha sehemu

salama, huwa hainipi shida kwa kuwa nimetoka kutafuta kwa ajili yake. ijumaa Wikienda: Unatamani mwanao afuate nyayo zako za kuwa msanii maana wewe ni msanii na baba yake ni director, kwa hiyo afuate nyayo za wazazi wake? linah: Siwezi kumchagulia mawanagu kazi ya kufanya, ni yeye tu akiwa mkubwa ataona nini afanye.

Kikubwa ni mimi kuongeza bidii kutafuta pesa ili niweze kumsomesha na pia niongeze bidii katika kumfundisha maadili ya dini na yanayohitajika katika jamii yetu ya Kitanzania. ijumaa Wikienda: Kuna siku nyingine huwa unaposti picha zako katika mitandao ya kijamii ukiwa na nguo ambazo zinaonesha maungo yako, hufikirii kuwa mwanao anakuwa na

mambo ya mitandao huwa yanajihifadhi kwamba akija kuyaona atakuchukuliaje wewe kama mama yake? linah: Mimi ni msanii kwa hiyo mavazi sidhani kama yana shida kwamba atakuja kunichulia kuwa ni mama wa aina gani, nafikiri kipindi hicho atakuwa ameshajua kazi ya mama yake kazi. Kwa hiyo sidhani kama itamuathiri chochote.

ijumaa Wikienda: Linah tunashukuru kwa ushirikiano wako na Ijumaa Wikienda linakutakiwa kila la heri katika malezi ya mwanao. linah: Asante sana, name ninalipenda Gazeti la Ijumaa Wikienda


Loading...

Toa comment