The House of Favourite Newspapers

Trafiki Kuwachapa Bakora Madereva Bodaboda, Waziri Abanwa – Video

Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe amesema kuwa bado kuna baadhi ya askari wa barabarani wamekuwa wakiwakimbiza waendesha boda boda na kuwachapa viboko.

 

Akiuliza swali bungeni leo Jumatatu Juni 17 2019, Mwambe amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwafanya waendesha bodaboda hao kuanguka na kuumia.

 

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni amesema hajaona wala kupata taarifa kuhusu polisi kuwachapa bakora waendesha bodaboda. “Hakuna taarifa tulizopokea kuhusu waendesha bodaboda kuchapwa viboko,”amesema Masauni.

 

Hata hivyo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Fatuma Tawfiq ambaye alitaka kujua kuhusu fidia na bima kwa watu waliojeruhiwa na kufa kutokana ajali, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema ameshatoa maelekezo ya bodaboda zinazotakiwa kupelekwa kituoni.

 

Ametaja makosa ambayo yanayotakiwa bodaboda kupelekwa kituo cha Polisi kuwa ni zile zilizohusika uhalifu, zisizo na mwenyewe na zilizohusika kwenye ajali.

 

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya Ndani kangi Lugola amesema;

“Kama ambavyo imeandikwa kwenye Biblia, kwamba siku ya kuja kwa Mwana wa Adam, Mwana wa Mungu aliye hai, hakuna ajuaye siku wala saa…nitaanza kutembelea vituo vya polisi…na ole wao nikute bodaboda hizi nilizokataza zimewekwa kituoni.”

Comments are closed.