The House of Favourite Newspapers

Kenya: Mwamamke Ashukiwa Kuwa na Ebola, Awekwa Chumba Maalum

Taarifa kutoka Ofisi ya Gavana Jimbo la Kericho nchini Kenya imesema imemweka mwanamke mmoja aliyeonesha dalili za ugonjwa wa ugonjwa wa Ebola katika chumba maalum katika Hospitali ya Kericho, iliyopo eneo la Bonde la Ufa Kusini – Magharibi mwa nchi hiyo.

Sampuli za damu za mgonjwa huyo zimechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na majibu yatatoka kati ya saa 12 hadi 24 zijazo.

 

Hakuna ripoti yeyote iliyotolewa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola karibu na mpaka wa Malaba isipokuwa katika eneo la Magaharibi mwa Uganda.

Comments are closed.