The House of Favourite Newspapers

Trump Alitaka Mwanasheria Ambaye Angebadili Matokeo ya Kura Georgia

0
Jeffrey Clark, ofisa wa Mahakama aliyetakiwa kuchukua nafasi ya Mwanasheria Mkuu Marekani.

ALIYEKUWA rais wa Marekani Donald Trump alikuwa na mpango wa kumfukuza mwanasheria mkuu kwa kukataa kubadili matokeo ya uchaguzi na kumweka ambaye angekubaliana na matakwa hayo.

 

Jeffrey Rosen,  aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mwanasheria Mkuu baada ya Bill Barr kujiuzulu muda mfupi kabla ya Krismasi, hakukubali maagizo ya rais huyo, kwa mujibu wa gazeti la New York Times.

 

Pia, Trump alimlazimisha Rosen kuteua washauri maalum akiwemo mmoja wa kusimamia upigaji kura (Dominion Voting Systems), mfumo wa upigaji kura ambao Trump na wafuasi wake waliulaumu bila ya kutoa ushahidi, alipodai kwamba walihamisha kura za Trump na kumpa Joe Biden.

 

⚫️ Kwa UPDATES, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply