The House of Favourite Newspapers

Tume ya Uchaguzi Yabadili Majina ya Majimbo Matatu

0

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imebadilisha kwa majina ya majimbo ambapo Jimbo la Chilonwa litaitwa Chamwino, Mtera linaitwa Mvumi na Kijito Upele lililopo Mjini Magharibi linaitwa Pangawe.

Mabadiliko yao yametangazwa na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage leo Julai 23, 2020 akiongea na Wanahabari ofisini kwake jijini Dodoma.

 

Ametaja idadi ya majimbo kuwa ni 264 Kama ilivyokuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo 214 yapo Tanzania Bara na 50 yapo Zanzibar na kata 3,956.

Pia ametangaza ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ajili ya Urais kuwa ni August 5 hadi 25, 2020.

 

Aidha, fomu za nafasi ya Ubunge na Udiwani zitatolewa kuanzia August 12 hadi 25, 2020.

Amesema fomu kwa ajili ya Urais zitatolewa katika Ofisi ya tume hiyo zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma na nafasi ya ubunge na udiwani zitatolewa katika Ofisi za uchaguzi zilizopo katika halmashauri na kata husika.

Leave A Reply