The House of Favourite Newspapers

Tumia Mshumaa Kuondoa MagagaMiguuni!

0

NI wiki nyingine tena mpenzi msomaji wa DONDOO ZA UREMBO tunakutana hapa kupeana elimu ya urembo.

Kutokana na wengi kulalamika kuwa na magaga (mipasuko miguuni) ambayo huleta athari mbalimbali kama kuchana mashuka, neti nk. Leo ninakuletea tiba ya tatizo hilo kwa kutumia mshumaa.

MAHITAJI

Mshumaa.

Mafuta ya mzeituni au ya nazi.

JINSI YA KUFANYA

Chukua mshumaa wako kisha ukwangue kama unavyokwangua karoti kwa kutumia kisu, weka kwenye bakuli ya udongo ule unga unaoupata. Baada ya hapo changanya na mafuta ama ya mzeituni au ya nazi vijiko vitatu, kisha chukua sufuria yenye maji ya wastani ibandike jikoni. Ikishapata moto, weka kibakuli hicho ndani ya maji na ukoroge mchanganyiko wako hadi mshumaa uyeyuke.

Baada ya kuchanganyika vizuri, epua mchanganyiko wako ukiwa bado wa moto na uanze kuyapaka miguuni. Unaweza kutumia tiba hii kila siku usiku kwa muda wa mwezi mmoja kisha utapata matokeo mazuri.

ANGALIZO

Wakati unaandaa tiba hii, hakikisha maji hayazidi urefu wa kibakuli na wala hayaingii kwenye mchanganyiko wako. Pia unapaswa kuvaa viatu vya kufunika kwa ajili ya kuzuia vumbi ukiwa kwenye mizunguko yako.

Leave A Reply