The House of Favourite Newspapers

Tunduma: Agizo la Rais Latekelezwa, Magari 1,000 Yakwama Mpakani

0

IKIWA ni siku moja tangu kuanza kutekelezwa kwa agizo la Serikali ya Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania, hali hiyo imesababisha magari ya mizigo kukwama kuendelea na safari zake.

 

Zambia ilianza utekelezaji wa agizo hilo Mei 11, 2020, kwa kufunga mageti yote mawili ya kuingilia nchini humo, maduka na shughuli zote zinazofanywa kwenye eneo la mpaka kutokana na agizo la Rais wa nchi hiyo, Edger Lungu ili kukabiliana na maambukizi ya Covid-19, hali iliyoibua vilio kwa wafanyabiashara wa mji wa Tunduma.

 

Wakizungumza baada ya utekelezaji wa agizo la kufunga mpaka, wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa wana mazingira magumu ya kumudu maisha yao kwani maisha ya mji wa Tunduma yanategemea sana biashara.

 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela, amefika katika mpaka huo uliopo mji wa Tunduma na kuwataka wasafirisha mizigo kuwa na subira.

 

Amesema kuna mazungumzo yanaendelea, na kwamba huenda mpaka huo ukafunguliwa mapema kufuatia makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Leave A Reply