The House of Favourite Newspapers

Rais Shein Atoa Tamko Kuhusu #Covid19

0

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa mikoa ya Pemba kuwatoa hofu Wananchi juu ya #COVID-19 na waendelee kujikinga kama walivyopewa maelekezo na wataalamu wa afya.

 

Amesema, yeye na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hawakuwa tayari kuzuia wananchi kusafiri na kufanya shughuli zao za kimaisha na badala yake waliwataka wananchi kuendelea kuelimishwa juu ya kujikinga na janga hilo.

 

Ameeleza kuwa wapo baadhi ya watu ambao hawatoi ushauri mzuri kwa serikali na wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya kuilazimisha serikali jambo ambalo  haiko tayari kulazimishwa katika kufanya wanavyotaka wao.

 

Amesisitizia haja ya kuendelea kuwahimiza wananchi kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono pamoja na kufuata taratibu zote za kinga zinazotolewa na wataalamu wa afya.

 

Leave A Reply