The House of Favourite Newspapers

Twaha Kiduku: Mwakinyo Anajibiwa Ulingoni

0

Global TV Online imefanya mahojiano na bondia Twaha Kiduku ambae hivi karibuni alishinda pambano na kujipatia gari na amezungumza mengi ikiwemo bifu lake na Bondia Hassan Mwakinyo.

 

“Unajua ninachoamini mimi ni nyodo tu, ushaona, kikubwa sitaki kufocus nayo kwa sababu zile clip nimeziona anataka ajibiwe ila mimi naendelea na mazoezi kwa sababu bondia wa kweli unapomtaka lazima akubali mpigane.

 

“Muwe kama wanaume, mnapigana maisha mengine yanaendelea mbele lakini kila siku inakuwa hivyo maana ugomvi wadada na wanaume ni tofauti, wadada mmoja anaweza akamshika mwenzie mara eehee sijui hivi na hivi…dela sijui la kuazima… eeh sijui hivi na hivi.

 

“Mnajibishana mwisho siku hata kushikana hamshikani ila wanaume mmoja anaweza akapewa tusi halafu mwingine akamvaa, sasa mambo hayo yakienda mimi na huo upande wa pili yatakuwa kama ya wadada…jamani hivi mara vile sasa mimi sipo hivyo, siwezi kuongea kama mtoto wa kiume ambayo anayaweza, anajua kazi yangu ni hivi basi mnapigana, mnaendelea.

 

“Lakini kuwa na magari, magari ndiyo ya kwake kama ana maghorofa ya kwake, watu hatutaki hayo sisi tunachotaka watu waone show hivyo tu, watu wanachotaka kuona ni ladha,” Bondia Twaha Kiduku.

Leave A Reply