The House of Favourite Newspapers

Nay wa Mitego, Imemuwakia

0

MWENYEWE anajiita Rais wa Kitaa pengine ndiyo maana wimbo wake mpya ameupa jina hilo.

Lakini zaidi anafahamika kama Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni aliachia wimbo huo ulijaa nondo za  kuikosoa serikali wengine kwa mambo ya tozo, bei ya sukari na sakata la wabunge 19 wa CHADEMA.

Wimbo huo ulipotoka tu, kuna watu walisema yaleyale aliyozoea kukutana nayo Nay yaani nyimbo zake za kiharakati kupigwa pini na Basata yatamkuta.

Tangu Agosti 30, watu wakaanza kusikilizia tamko la serikali, hali imekuwa tulivu na ngoma inazidi kutusua kwenye mitandao ya kijamii.

Hapo sasa lile suala la nyota njema kumuwakia msanii huyo likaanza kuwaingia watu wakilini.

Kila ukifikiria wimbo huo unaona kama msela amejaa bahati, KWANZA ameweza kupenya kwenye mikono ya serikali mpaka sasa.

PILI ametoboa ngozi ngumu YouTube na kushika namba MOJA kwenye trendi akitumia mtaji wa wafuatilia wake 298 tu.

Wimbo wake huo umeweza kuzishinda nyimbo kama Teacher wa Harmonize mwenye wafuatliaji Mil 2.75, Happy Birthday wa Rayvanny mwenye wafuatiliaji Mil 3.13 na wasanii wengine kibao ambao nyimbo zao zimeshika adabu kwa Rais wa Kitaa.

Hata Nay mwenyewe huko aliko anasema “Ni Mungu ambaye kaniangazia hii nyota.”

@manyota_rich

Leave A Reply