The House of Favourite Newspapers

Twanga Ilivyozindua Albam ya 14 Kibabe, Mashabiki Full Vibe, Nyomi Kama Lote

0
Mashabiki wakiwa ‘full mzuka’ kwenye onesho hilo.

Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ usiku wa kuamkia leo imezindua albam yake ya 14 iitwayo Mapenzi Sigala Kali “Inawaka mbele na nyuma” huku nyomi kubwa la mashabiki likihudhuria na full vibe.

Papii Kocha (kulia) na baba yake Nguza Viking a.k.a Babu Seya wakikamua katika maonesho ya utangulizi.

Uzinduzi huo umefanyika Ukumbi wa Break Point uliopo Kijiji cha Makumbusho Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Pauline Gekul.

Super Nyamwela (kushoto) akiwaongoza wanenguaji kushambulia jukwaa.

Twanga kama ilivyo kawaida yao kuingia na sapraiz waliingia na vazi la kiasili na kusababisha mashabiki watumie muda mwingi kutafakari kuanzia mavazi mpaka shoo yenyewe kisha baadae ndipo wakaanza kubadilisha mavazi tofauti na kuinogesha shoo hiyo.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Pauline Gekul akizungumza kwenye uzinduzi huo,kushoto ni mmiliki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kuwatunukiwa tuzo ya keshima wanamuziki waliotukuka wakiwemo walioaga dunia.

Mtoto wa marehemu Aisha Madinda akionesha tuzo ya heshima aliyotunukiwa mama yake.

Walioibuka na tuzo hizo ni King Kikii, Hassan Bitchuka, Luiza Mbutu na waliopewa tuzo hizo wakiwa wameaga dunia ni pamoja na Abuu Semhando, Banzastone, Mbaraka Mwishehe, Marijan Rajab, TX Moshi William, Aisha Madinda, Ruge Mutahaba, Mcd Tumba na wengineo.

Mwanamuziki Chaz Baba (kulia) akiongoza mashambulizi jukwaani.

Shoo hiyo iliacha gumzo huku wengi wakipiga mayowe wakitaka irudiwe “irudiweeeee…” Ndiyo mayowe yaliyosikika.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS GPL   

Leave A Reply