Twiga Waapa Kubeba Ubingwa wa Cosafa

WACHEZAJI na benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars wamesema kuwa kuna asilimia 80 ya kuwashinda Malawi na kutwaa kombe la Cosafa.

 

Twiga Stars leo majira ya saa 10:00 alasiri, watacheza mchezo wa Fainali dhidi ya Malawi, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia wanafika kwenye hatua hiyo

 

Twiga walitinga fainali hiyo baada ya kuwachapa Zambia kwa penati 3-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

 

Kocha wa timu hiyo Bakari Shime aliliambia Championi kuwa: “kazi kubwa msimu huu itaonekana ya thamani zaidi kama tutapata matokeo kwenye mchezo huu wa fainali Imani yangu inasema tutashinda”

 


Toa comment