The House of Favourite Newspapers

Twitter Yatishia Kuishtaki Kampuni ya Meta Kisa App Yake Mpya ya Threads

0

 

Twitter imetishia kuishtaki kampuni ya Meta juu ya app yake mpya ya Threads ambayo inafanana na app ya Twitter, sababu za kuishtaki Meta ni wizi wa wafanyikazi wa Twitter, pamoja na wizi wa siri za kampuni ya Twitter.

Nukuu ya barua iliyotumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Meta na Facebook Mark Zuckerberg na wakili wa Twitter Alex Spiro imeeleza:

“Twitter inakusudia kutekeleza kwa dhati haki zake za uvumbuzi, na inaitaka Meta kuchukua hatua za haraka kuacha kutumia siri zozote za biashara za Twitter au habari zingine za siri,”

“Twitter inahifadhi haki zote, ikiwa ni pamoja na upekee wake, ufichuzi, au matumizi ya haki miliki yake na app nyingine.”

Siku ya Alhamisi Meta ilizindua Threads mtandao ambao unaonekana kuwa mpinzani mkubwa na tishio kwa Twitter. Threads ndani ya saa 24 ilivunja rekodi ya kuwa na zaidi ya watu milioni 40 waliojisajili.

WAZIRI MAKAMBA AIBUA MAPYA – “BWAWA la MWALIMU NYERERE LIMEPITILIZA KUJAA MAJI”

Leave A Reply