Tyson Fury Amchapa Wilder Tena

BONDIA Tyson Fury amempiga Bondia Deontay Wilder kwa KO Katika Raundi ya 11 na kutetea ubingwa wake wa WBC katika pambano liliopigwa leo T Mobile Arena, Nevada nchini Marekani.

 

Hili lilikuwa pambano la tatu kukutana kwa mabondia hao ambapo mara ya kwanza walitoka sare mwaka 2018, kabla ya Fury kushinda mwaka 2020 na leo ameshinda tena.

 

Mpaka sasa Fury raia wa Uingereza mwenye miaka 33, amepigana mara 32, ameshinda 31 na sare 1. Wilder sasa amepigana mara 45, amesinda 42, sare 1 na kupigwa mara 2.


Toa comment