Ubingwa wa Mtibwa Mapinduzi Waondoka na MO Simba

USIKU wa kuamkia leo Simba imepoteza taji la kwanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, katika fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

 

Hata hivyo, wakati mashabiki na wapenzi wa Simba wakiugulia maumivu kwa kipigo hicho, mambo yamezidi kuharibika zaidi baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo) kutangaza kuachia ngazi kutokana na kutoridhishwa na matokeo hayo.

Katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mo alisema: “Baada ya kulipa mishahara inayofikia Sh4 bilioni kwa mwaka, najiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Nitabaki kuwa mwekezaji na nitazingatia kukuza miundombinu ya soka la vijana.”

Mtibwa ambao walionekana kucheza soka safi na kumiliki mchezo huo, ilipata bao lake la ushindi dakika ya 38 kupitia kwa Awadh Salum, ambaye alipenya katikati ya msitu wa walinzi wa Simba.

Uamuzi wa Mo kuachia wadhifa huo Simba, umeibua sintofahamu sio kwa wanachama tu, bali kuhusu pia hatima ya bodi hiyo.


Loading...

Toa comment