The House of Favourite Newspapers

Ubingwa Wanukia Jangwani, Takwimu Hizi Hapa

0

Klabu ya Yanga imekuwa na nafasi kubwa sana msimu huu wa kuweza kutwaa ubingwa wa NBC Premier League hali hii imeonekana baada ya klabu hiyo kuanza vizuri sana toka mwanzoni mwa msimu huu hadi sasa licha ya kuanza vizuri laikini pia wakiwa na wachezaji bora sana katika kikosi chao.

 

Klabu ya Yanga Sc hadi sasa imecheza michezo 13 na kuvuna alama 35 na kupotenza alama 4 tu katika michezo yake ambapo wapinzani wao Simba Sc wakiwa wamecheza michezo 13 na kuvuna alama 25 huku wakiwa wamepoteza alama 14 kwa takwimu hizi Yanga wamekuwa na nafasi kubwa sana hadi sasa kuweza kutwaa ubingwa msimu huu wakiwa wanamuombea mpinzani wao aendelee kufanya vibaya katika mechi zake zijazo.

 

.
Klabu ya yanga Sc kwa sasa ndio timu pekee inayoonekana kufanya vizuri sana ukilinganisha na timu zingine katika NBC premier League ambapo imekuwa na wachezaji wazuri sana na wakuelewana katika kila idara sio beki sio viungo sio washambuliaji wote wwameonekana kupambana sana wakiwa uwanjani na kuweza kusaka alama tatu kwa pamoja ambapo hali hii inawafanya Yanga kuonekana kuwa bora sana katika msimu huu wa 2021- 2022.

 

Kunukia kwa ubingwa Yanga ni pamoja na wapinzani wao kuonekana kufanya vibaya sana katika michezo yao huku wakiendelea kuwa na matokeo mabaya ambapo wameweza kupoteza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar bao 1-0 huko mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba.

 

Simba Sc wamepoteza mchezo huo lakini huku wakiwa wamepata nafasi nyingigi sana na kushindwa kuzitumia hasa kipindi cha kwanza ambapo hawakuweza kufungana, lakini pia Simba Sc bado ina nafasi ya kushindania taji ilo kwa sababu bado wana kikosi kizuri na wanaweza kufanya madiliko katika michezo yao ijayo.

 

Kwa sasa mashabiki wa Simba Sc wamekuwa ni watu ambo wamekuwa kwenye huzuni kubwa sana juu ya hali wanayoipitia kwa sasa wamekuwa ni watu wa kujiuliza maswali mengi sana juu ya timu yao huku wakiwa wanakosa majibu, mashabiki hao ambao hawajazoea hii hali kwa misimu minne mfululizo wakiwa ni watu wakufurahi mda wote huku wapinzao wao wakiwa na huzuni wakati je mwaka huu ni zamu yao Simba Sc au muda bado yote yanawezekana.

Leave A Reply