The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi Mkuu: Dkt. Bashiru Azindua Kituo cha Mawasiliano CCM

0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Bashiru akiwasiliana na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, kwa simu iliyopigwa kwenye kompyuta mpakato (Laptop) ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha CCM kuhusu Habari za Uchaguzi kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo. 

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bashiru Ally Kakurwa leo Agosti 17, 2020 amezindua kituo cha mawasiliano kuhusu habari za uchaguzi kilichopo kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Dk. Bashiru akitazama picha za wagombea urais kupitia CCM zilizopambwa upenuni mwa kituo hicho. Wagombea hao ni Dk. John Magufuli anayewania urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea urais Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi.

 

Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, Gabriel Athuman akiangalia mpangilio ulivyo ndani ya kituo hicho.

 

Afisa Tehama wa CCM, Magoti Wambura akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru, jinsi wanavyowasiliana na viongozi, wanachama na umma kupitia kwenye kompyuta mpakato wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha habari za uchaguzi.

 

Dk. Bashiru akikagua kituo hicho na kupata maelezo kutoka kwa Afisa Tehama, Wambura (kushoto). Kulia ni Gabriel Athuman.

 

Afisa Tehama wa CCM, akitoa maelezo kwa Dk. Bashiru jinsi kituo hicho kitakavyopokea taarifa mbalimbaliza za uchaguzi kupitia kituo hicho.

 

Dk Bashiru akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ambapo alisema kuwa hivi sasa kituo hicho kitakuwa kinakusanya taarifa mbalimbali za uchaguzi kutoka kwa viongozi wa CCM, Wanachama na Umma na baada ya uchaguzi kazi yake kubwa itakuwa kukusanya Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

 

Mtumishi wa kituo hicho, Debora Kiyuga akiwa tayari ameanza kazi ya mawasiliano

 

Baadhi ya watumishi wakiwa kazini kituoni hapo

 

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.

Leave A Reply