The House of Favourite Newspapers

UCHAGUZI RWANDA: KAGAME ANATARAJIA KUTAWALA KWA MUHULA WA TATU

0
UCHAGUZI RWANDA: KAGAME ANATARAJIA KUTAWALA KWA MUHULA WA TATU
Kagame

RWANDA inakwenda kupiga kura huku Paul Kagame akitarajiwa kushinda katika awamu hii ya tatu.

 

Kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 59, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Frank Habineza wa ‘Democratic Green Party of Rwanda’, pia upinzani mwingine upo kwa mgombea binafsi, Philippe Mpayimana.

 

Kagame anapongezwa kwa kuinua uchumi wa Rwanda tangu alipoingia madarakani mwaka 2000.

 

Hata hivyo wapinzani wanamkosoa kwa kuminya uhuru wa demokrasia nchini humo.

 

Zoezi la upigaji kura litaanza saa 01.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00 jiioni.

 

Mwaka 2015 katiba ya Rwanda ilifanyiwa marekebisho, ikampa Rais Kagame nafasi ya kutetea kiti chake mpaka mwaka 2034.

 

Wapinzani wametoa malalamiko kuwa wafuasi wao wamekuwa wakikutana na vitisho mbalimbali.

 

Hata hivyo, chama tawala kimepinga tuhuma hizo.

Leave A Reply