The House of Favourite Newspapers

Ufafanuzi Anayejiita ‘Prof. Mohamed Janabi’ Mitandaoni

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof. Mohammed Janabi.

 

TAASISI  ya Moyo  Jakaya Kikwete imewajulisha wananchi kuwa wazipuuze taarifa zinazotolewa kupitia ukurasa wa Twitter wa mtu anayejiita Prof. Mohamed Janabi kwani  si za kweli na hazitolewi na Prof. Janabi.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC),Prof. Mohamed Janabi, inasema yeye hana akaunti yoyote ya mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, Facebook, Instagram na Youtube.

 

Imesema Prof.  Janabi hutoa taarifa kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo, magonjwa ya moyo na afya kwa jumla kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ya taasisi ambayo ni Youtube kwa jina la Taasisi ya Moyo TV, Twitter, Facebook na Instagram kwa jina la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

 

Taarifa hiyo inatoa “onyo kwa watu wote wanaojihusisha na akaunti hiyo batili na wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria. Aidha, Taasisi inatoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na akaunti hiyo batili kwa kuwa taarifa zinazotolewa siyo sahihi.”

Leave A Reply