The House of Favourite Newspapers

Ufaransa Yampongeza JPM Kuingia Uchumi wa Kati

0

BALOZI  wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier, leo Desemba 2, 2020, amemkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi, barua toka kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyomwandikia Rais  John Magufuli kumpongeza kwa kuiwezesha Tanzania kuingia uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda tarajiwa.

 

Julai Mosi mwaka huu Benki ya Dunia iliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati, hatua ambayo  imefikiwa mapema zaidi tofauti na muda uliotarajiwa.

 

Mataifa yenye kipato cha kati ya dola 1,006 hadi dola 3,955 kwa mtu mmoja hutajwa kuwa mataifa yenye kipato cha kati, lakini yaliyo na uchumi mdogo huku yale yenye kipato cha kati ya dola 3,956 hadi dola 12,235 yakidaiwa kuwa mataifa yenye kipato cha kati yenye uchumi unaoimarika.

Leave A Reply