Ufaransa yashinda bila Mbappe, Pogba

TIMU ya Taifa ya Ufaransa ikiwa bila kiungo wake mahiri, Paul Pogba na mshambuliaji Kylian Mbappe juzi ilionyesha kiwango cha juu na kufanikiwa kuichapa Albania, mabao 4-1.

 

Ufaransa wakiwa nyumbani kwenye mchezo huo wa kufuzu Euro ilifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu. Kiungo Kingsley Coman, alifanikiwa kufunga mabao mawili kwenye mchezo huo, huku mengine yakifungwa na Olivier Giroud na Jonathan Ikone.

 

Matokeo haya yanawafanya Ufaransa kujiweka kwenye sehemu nzuri ya kufuzu kwa fainali hizo za mwaka 2020.Pogba pamoja na Mbappe walionekana wakiwa jukwaani wakitazama mchezo huo huku mara kwa mara wakijadiliana baadhi ya mambo.

 

Hata hivyo, mechi hiyo ilichelewa kuanza kwa dakika saba baada ya makosa kufanyika badala ya kupigwa Wimbo wa Taifa wa Albania ukapigwa wa Andorra, ambapo wachezaji wa Albania waligoma kucheza hadi wimbo wao upigwe.


Loading...

Toa comment