The House of Favourite Newspapers

Ujenzi wa Barabara ya Mikumi- Ifakara Kwa Kiwango cha Lami Wafikia Asilimia 86

0

Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Kitaifa Mkoani Morogoro ikiwemo Ujenzi wa Barabara ya Mikumi – Kidatu – Ifakara (sehemu ya Kidatu – Ifakara, (km 66.9) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu ambao umefikia asilimia 86% za utekelezaji na tayari Mkandarasi amekamilisha km 55.67 za lami kati ya km 66.9 zinazotakiwa kwa mujibu wa Mkataba.
Pia inaendelea na Ujenzi wa barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 142) kwa kiwango cha lami (sehemu ya Rudewa – Kilosa km 24) kwa kutumia fedha za ndani; Mkandarasi amekamilisha ujenzi wa kilometa 22.05; barabara imekabidhiwa na inatumika, Mkandarasi amekamilisha pia madaraja matatu ya Kobe, Wailonga na Mazinyungu na kwasasa anaendelea na kazi ya km 0.75 ya maungio ya madaraja hayo.
Msimamizi Mkuu wa Matengenezo ya barabara na madaraja TANROADS Mkoa wa Mororgoro Mha. Patrick Rambika ameeleza hayo tarehe 6 Machi 2024 alipozungumza na kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya miundiombinu ya ujenzi wa barabara na madaraja.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (Kizuka Army Camp), 11.6km – Mradi umesainiwa tarehe 7 Februari 2024, Mkandarasi Mzawa, M/s Kings Builders Ltd atatekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 20.54 kwa muda wa miezi 12.
Amesema mradi wa Ujenzi wa barabara ya Bigwa – Kisaki; sehemu ya Bigwa –Mvuha, km 78; Mkataba umesainiwa tarehe 5 Februari 2024, na Mkandarasi M/s China railways 15 Bureau Group Corporation ya China atatekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 132.016 kwa muda wa miezi 27.

Leave A Reply