The House of Favourite Newspapers

Ujio wa Ramsey Nouah; Mama Kanumba Kilio Upya!

BAADA ya staa wa Filamu za Ki-Nigeria (Nollywood), Ramsey Nouah kuzuru kaburini kwa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba kwa mara ya kwanza, imekuwa simanzi nzito tena kwa mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa ambaye ameangua kilio upya kaburini hapo.

 

Wakiwa makaburini hapo mapema leo, Ramsey na Mama Kanumba walitumia muda mwingi kukumbatiana na kulia kwa huzuni jambo lililoteka na kuvuta hisia za watu wengi. Mbali na tukio hilo, Ramsey alizidisha machungu kwa mama huyo baada ya kuanza kutamka maneno kama anazungumza na marehemu Kanumba ambapo alimueleza mambo yenye kuumiza.

“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,” alisema Ramsey katika mazungumzo yale na Kanumba aliyoyatoan kwa hisia kali hali iliyomsababishia Mama Kanumba maumivu makali.

Full Video: Ramsey Noah Amwaga Machozi Kwenye Kaburi la Kanumba

Comments are closed.