The House of Favourite Newspapers

Ujue Umasikini Usiozaliwa Nao

markettanzania_hor_misd-e1471356940678

Wananchi wa Tanzania wakiwa sokoni.

Hali ngumu ya maisha kwa sasa imenisukuma kukuandikia haya mpenzi msomaji.  Kukomesha umasikini wa kupindukia ni hatua muhimu sana, sio tu kwa sababu ya kuwahurumia watu masikini hapana bali  uchumi wa dunia utanufaika sana kutokana na mchango wa wale watakaonyanyuka kupiga vita utegemezi wa misaada. Watu masikini wanapopewa uwezo kisheria ulimwengu unakuwa umepata silaha ya kuendeleza vita dhidi ya umasikini.

Kabla ya kuumulika umasikini na athari zake katika jamii tujikumbushe busara za Mwalimu Nyerere katika falsafa yake ya “Kazi na Kujitegemea” aliposema “Umasikini Ni  Gharama Sana.”

dsc03321

Je Umasikini ni nini?

Hali ya ukosefu wa mahitaji muhimu ya binadamu ni kipimo cha awali cha umasikini na ndio maana ya msingi ya umasikini. Umasikini hauishii katika kipimo cha ukosefu wa mahitaji tu bali mawanda yake ni mapana kiasi ambacho kipimo cha umasikini kinapimwa katika kupata huduma za kijamii kama vile elimu na afya bora.

Hakuna jamii isiyo na umasikini, kipimo cha  maendeleo hupimwa kuangaliwa kiwango cha umasikini. Kwa nchi zinazoendelea na zisizo endele kuna tofauti ya kiwango cha umasikini, nchi zinazoendelea umasikini huathiri kaya moja kwa moja. Ukosefu wa chakula, malazi na mavazi huu ndio  umasikini wenye umri mkongwe kwa nchi zilizoendea kama Tanzania.

Kutoka kwa wakoloni waafrika tupandikizwa mbegu ya umasikini, umasikini wa utegemezi yaani bila wao hatuwezi kulikamilisha jambo lolote la kujikwamua kiuchumi bila ya wao. hali hii ya utegemezi ndio umasikini usiozaliwa nao.

stonezenj

Utegemezi si jambo baya bali utegemezi uwe na malengo ya leo nategemea, kesho nitajitegemea na kesho kutwa nitategemewa. Ukiwa na mawazo ya namna hii kichwani hauwezi kuwa na umasikini usiozaliwa nao. Ubongo wenye utegemezi kamwe hauwezi kuleta kasumba chanya katika jamii, ubongo huo hauwezi kutatua tatizo bala yake utalikimbia tatizo, ubongo wa namna hiyo hautamudu kufanya  maamuzi binafsi badala yake utakuwa wa kuamuliwa na wengine.

Kuepuka umasikini usiozaliwa nao njia pekee ni kufuta wazo la utegemezi katika mawazo yako. Mfano ndoa nyingi zimekosa amani na kuishia matatani kutokana na hali ya utegemezi. Wanafunzi wengi wameshindwa mitihani kutokana na hali ya utegemezi. Hivyo basi utegemezi ni chanzo halisi cha umasikini usiozaliwa nao.

(Habari na Salum Milongo, GPL)

Comments are closed.