The House of Favourite Newspapers

Ujumbe wa Mahaba wa Ben Pol Kwa Bethidei ya Mpenzi Wake

 

MSANII Bernard Paulo maarufu kama Ben Pol ameandika ujumbe wa mahaba katika akaunti yake ya Instagram ambao ameuelekeza kwa mpenzi wake, Anerlisa toka Kenya, ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo Juanuari 9.

 

Ben Pol ameweka picha moja na video mbili ambazo zilikuwa zimeambatana na maneno yanayosomeka, “Happy Birthday My Love @anerlisa .. Words Cannot Explain How Much I Love You (Maneno hayawezi kueleza jinsi gani navyokupenda) 💞, Nakutakia Maisha Marefu Na Furaha. May All Your Dreams Come True..(nakuombea ndoto zako zitimie) #MyQueen 🙏🏽❤😘💞💕”ameandika Ben Pol

 

Lakini  mpenzi wake huyo alijibu kwenye sanduku la maoni kwa kuandika: “Thank you my love. I love you too very much. To more years together.”

 

Comments are closed.