Magufuli Ampa Mtihani Waziri wa Madini: “Mnataka Nijiteue Kuwa Waziri?”

RAIS John Magufuli amemuagiza Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko, kuhakikisha anajenga vituo vya madini vitakavyosaidia kuratibu biashara ya madini hayo ili Serikali isipoteze mapato yake na wananchi waweze kunufaika.

 

Rais Magufuli akimkabidhi vitendea kazi, Doto Biteko alipoapishwa kuwa Waziri wa Madini. Kabla ya Uapisho huo Mhe. Biteko alikuwa Naibu Waziri wa Madini. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2019

 

Magufuli amesema hayo leo Jumatano, Januari 9, 2019 baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana akiwemo waziri huyo na aliposlema  sekta ya madini bado ina changamoto kubwa na kwamba nchi inayoongoza kwa Afrika Mashariki kwa kuuza dhahabu siyo Tanzania japo ndiyo mzalishaji mkubwa.

Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu Dkt. Steven James kuwa mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma.

 

“Dhahabu yetu hailinufaishi taifa, Wizara ya Madini tumewahi kujiuliza madini yanayochimbwa yanaenda kuuzwa wapi? Najua kwenye sheria inatakiwa kuanzishwa kwa ‘mineral centres’ lakini tujiulize, zimeanzishwa ngapi? Ziko wapi? Inauma ukiona zaidi ya kilo 300 zinasafirishwa. Je, zimesafirishwa ngapi?

Rais Magufuli akimuapisha George Daniel Yambesi kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma.

 

“Ndio maana nafukuza hata mawaziri siyo kama siwapendi, wengine ni marafiki zangu, lakini utafanya nini sasa lazima tufanye kazi. Mimi nitaendelea kufanya mabadiliko kila mahali, ambapo nitakuwa sijaridhika; anayehusika ataondoka, hata Biteko nimekuteua lakini nikiona haparidhishi utaondoka. Kama mtu hawajibiki anaondoka tu, Tume ya Madini ikafanye kazi, lazima tuanzishe vituo vya madini kila mahala ili udhibiti wa madini uwe wa hali ya juu.

Magufuli akimuapisha Yahaya Fadhil Mbila kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma.

 

Rais alimwagiza Biteko kuanzisha mfumo wa vituo hivyo  huko Geita na maeneo mengine akimwelekeza kushirikiana na Wizara ya Fedha  na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ili kuanza kununua dhahabu nchini.

Aliyesema hayo kutokana na kutokuwepo kwa uratibu wa jinsi dhahabu hiyo inavyopatikana na mahali inapouzwa, ambapo sehemu kubwa huuzwa na kutoroshwa na wafanya magendo na kuifanya serikali kutojua mzunguko mzima wa dhahabu hiyo.

Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Bi. Dorothy Mwaluko alipoapishwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji). Kabla ya Uapisho huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 

 

Alisisitiza kwamba pakiwepo mfumo thabiti wa kufuatilia uzalishaji na uuzaji wa dhahabu kwa kupitia vyombo vya serikali, madini hayo yanaweza kutumika kama njia ya kurudisha thamani ya shilingi nchini.

Loading...

Toa comment