The House of Favourite Newspapers

Ukikamata Wafungwa Hawa Unapewa Zawadi ya Bilioni 1.23

0

MAMLAKA nchini Kenya imetangaza zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazosaidai kukamatwa kwa wafungwa “hatari” waliotoroka jela walimokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma zinazohusiana na ugaidi.

 

Watatu hao ni Mohamed Ali Abikar, Musharaf Abdalla,na Joseph Juma Odhiambo. Mmoja wao, Abikar alihusika katika shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa April 2, 2015 ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya wanafunzi 100.

 

Abdalla alikuwa anazuiliwa kuhusiana na shambulio lililofeli katika bunge la Kenya na Odhiambo alikuwa amekamatwa kwa kuwasajili vijana katika kundi la wanamgambo wa al-Shabab, ilani iliyotolewa na polisi ilisema.

 

Wafungwa hao walitoroka kutoka kwa Gereza Kuu la Kamiti viungani mwa mji mkuu, Nairobi, Jumatatu saa 01:00 kwa saa za huko.

 

Polisi wanatoa zawadi ya shilingi milioni 60 za Kenya sawa na ($535,000: Tsh bilioni 1.23) kwa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa wote watatu.

 

Kenya imewahi kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyopangwa na kutekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab.

Leave A Reply