The House of Favourite Newspapers

ULAYA HAKUKALIKI: JOTO KALI LATISHIA UHAI

0
ULAYA HAKUKALIKI: JOTO KALI LATISHIA UHAI
Pori likiwaka moto

Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea kwa sababu ya shughuli za binadamu ikiwemo ongezeko la viwanda, joto kali limegeuka tishio katika baadhi ya maeneo barani ulaya. Mataifa mbalimbali yanatoa tahadhari kwa wakazi wake kuhusu hatari ya kuongezeka kwa joto.

 

Nchini Italia hali ni mbaya, joto limesababisha moto porini, na baadhi ya miji hivi sasa ipo katika tahadhari. Mbali na moto huo, ukame unaikabili baadhi ya miji.

ULAYA HAKUKALIKI: JOTO KALI LATISHIA UHAI
Mwanamume akipoza kichwa kupunguza joto huko Roma

KIASI CHA JOTO KILICHOFIKIWA

Katika miji ya Sardinia, Sicily, na Roma, joto limefikia mpaka 42C. wanachi katika maeneo hayo wameshauliwa kusalia majumbani na kunywa maji mengi.

 

Kutokana na matukio hayo, hali ya tahadhari imetangazwa katika miji 26 ulaya.

 

Leave A Reply