The House of Favourite Newspapers

Ulinzi Simba, Yanga Kesho Taifa Usipime – Video

0

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema hakutakuwa na nafasi ya uhuni wa aina yoyote kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Yanga utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, kwani ulinzi umeimarishwa kwa asilimia kubwa.

 

Hayo yalisemwa jana Alhamisi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Ibrahim Mwayela katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya TFF, Karume Ilala jijini Dar.

 

Akizungumzia maandalizi kuelekea katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, Mwayela alisema wamefanya maboresho kadhaa ya kiusalama ikiwemo suala la ulinzi kwani hawataki kuona mashabiki wakipata tabu kuingia uwanjani, pia wamefanya hivyo ili kudhibiti wale wote wanaokwenda uwanjani kwa lengo la kuanzisha vurugu na kuwasumbua mashabiki wakati wa kuingia uwanjani.

 

“Awamu hii ulinzi umeimarika kwa asilimia 100 kuelekea katika mchezo huu, vikao mbalimbali bado vinaendelea kufanyika ili kuhakikisha mchezo unafanyika kwa kufuata kanuni za ndani na nje ya uwanja na ndiyo maana hata vyombo vya ulinzi tumekuwa tukivishirikisha katika mipango yetu ili kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa katika mchezo huo.

 

“Tiketi zimeshaanza kuuzwa na utaratibu maalumu wa namna ya kuingia uwanjani umeshapangwa, suala la viingilio lipo wazi na hata waamuzi wa mchezo wote wapo tayari, rai yangu ni kwa mashabiki kuwahi mapema uwanjani na kufuata utaratibu ili kuwarahisishia watu wa usalama kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa, kwa jumla maandalizi yote kwa upande wa bodi ya ligi yameshakamilika na mechi itaanza saa 11 kamili jioni,” alisema Mwayela.

Leave A Reply