The House of Favourite Newspapers

UMEINYAKA HII YA MWARABU KWENDA SAUZI KUFANYA KAZI NA ZARI?

DAR ES SALAAM: Mwanamama, raia wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemtosa kweupe aliyekuwa bodigadi wa mwanamuziki huyo, Suleiman Mkundi almaarufu Mwarabu Fighter.

 

Wikiendi iliyopita Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi alitua Bongo akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ anakoishi na familia kwa ajili ya shughuli za kibalozi. Katika shughuli zake hizo kuanzia alipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar alikuwa akilindwa na Mwarabu Fighter na mwenzake.

 

Katika mazungumzo na Gazeti la Amani, Mwarabu Fighter alisema kuwa yupo tayari kwenda na Zari nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kumlinda kwa kuwa wanafahamiana vizuri, jambo ambalo lilikuwa tofauti kwa mwanamama huyo.

 

“Mimi hata leo nipo tayari kwenda South Africa kwa ajili ya Zari, nipo tayari kufanya naye kazi kwa sababu tunafahamiana vizuri na ni mtu mzuri,” alisema Mwarabu ambaye alishindwana na Mondi na kuongeza;

 

“Najua ni kwa kiasi gani anahitaji ulinzi na yeye anajua ni kwa kiasi gani ninajua kazi yangu hii ya kulinda mastaa.”
Wakati Mwarabu Fighter akisema hivyo, Gazeti la Amani lilimgeukia Zari na kumuuliza uwezekano wa kumchukua jamaa huyo kwa ajili ya ulinzi ambapo alisema kwa kifupi;

 

“Hapana, siwezi.” Alipoulizwa kwa nini, Zari hakutaka kuweka wazi sababu za kumtosa Mwarabu Fighter aliishia kucheka.

 

Stori: Imelda Mtema, Amani

BINTI ATESEKA MIAKA 6 KITANDANI/maumivu ya nyonga yalemaza mguu

Comments are closed.