The House of Favourite Newspapers

Umeumizwa, acha yapite, maisha lazima yasonge-2

0

stressed-womanHongera sana mpenzi msomaji kwa kuifikia, kuifurahia na kuimaliza Sikukuu ya Krismasi vizuri ni jambo jema sana na la kumshukuru Mungu.

Niwape faraja na tumaini jipya wale wote wanaofunguka kutokana na makala za uhusiano kupitia safu yetu hii pendwa ya XXLove.

Yafuatayo ni sehemu ya maoni yenu wapenzi wasomaji yaliyotokana na mada yetu ya wiki iliyopita ya ‘Umeumizwa, Acha Yapite, Maisha Yasonge’.

MSOMAJI WA MBEZI BEACH, DAR
Mada nzuri sana, inafundisha, mimi ni mfano; nilikuwa na mchumba wangu tuliyependana ila nilipopata matatizo alinisaliti na kuchukuliwa na mtu mwingine. Hivi sasa amepewa ujauzito. Pamoja na matatizo yangu hanipigii simu wala kutuma ujumbe.

NAITWA EVA JONAS
Mwandishi Mungu akupe maisha marefu, XXLove imenibadili fikra na akili yangu, nilikuwa mtu wa kulia na kuwaza kila siku. Lakini niliposoma mada ya wiki iliyopita nimekuwa mpya kabisa.

JINA KAPUNI
Nimependa mada yako, mimi ni mama wa mtoto mmoja, nina mwaka mmoja kwenye uhusiano ila kwa sasa nimetokea kumchukia mume wangu, hata hamu ya kuwa naye faragha sina, hisia inakuwa ndogo, nifanyeje?

WARDA WA DAR
Nimeishi na mume wangu lakini hivi karibuni kaniacha yapata mwaka sasa, nashindwa kuzoea, nahitaji kuonana na wewe, nina mengi nahitaji unishauri.

JINA KAPUNI- MBAGALA, DAR
Mtaalam kuhusu mzazi mwenzangu, mpaka leo kimya ila nimependa sana mada yako, imenifariji, mapenzi yanaumiza ila kikubwa ni kukubaliana na hali halisi.

BINTI WA KITANGA
Nilishaumizwa sana na hapa nilipofikia sihitaji mwanaume yeyote, najihisi nina nuksi, nimetendwa na wanaume wanne, nifanyeje mtaalam?

MAMA WA FAMILIA
Mimi ni mama wa mtoto wa miezi sita, nimeolewa na nilikuwa namuamini sana mume wangu, juzi nimegundua kuwa tuko wanawake wanne au watano katika uhusiano, kiukweli roho yangu imemkinai sana, namchukia kweli.Mada yako imenifurahisha sana, umenitia moyo kweli, sasa nifanyaje ili aniache?

JINA KAPUNI
Hongera kwa kutuelimisha, naomba unisaidie; mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21, nilizaa na jamaa f’lani, cha ajabu mwenzangu alianza kubadilika, ghafla akakata mawasiliano, nilishamuomba sana msamaha lakini alikataa, ndugu walinitenga kisa yeye, kibaya zaidi moyo wangu hauko tayari kumsahau na kumpenda mwingine.
Labda alinikimbia kwa sababu ya ujauzito, kama ndivyo basi aje tulee mtoto wetu, ninaomba ushauri.

ROSE WA DODOMA
Nimefarijika sana, mimi ni mmoja wa wanawake niliyepita mateso ya mapenzi, yanaumiza sana, unaweza kumpenda mwanaume ukajidanganya ni wako peke yako kumbe mwenzio ana fikra zake.

Leave A Reply