UMEYASIKIA YA Zabibu Kiba kwa Banda?

KWELI inapofika kwenye suala la mapenzi kila mmoja anatulia! Dada asiyependa makuu kwenye mitandao ya kijamii ambaye pia ni dada wa staa wa Bongo Fleva, Alikiba, Zabibu Kiba ameamua kuweka wazi penzi lake kwa mumewe ambaye ni msakata kabumbu wa 88888 ya nchini Afrika Kusini, Abdul Banda kuwa anaona kama kamuoa jana tu.

 

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Zabibu alisema kwa sasa tayari wameshafikisha mwaka mmoja wa ndoa na mumewe huyo lakini ukweli ni kwamba anaona kama amemuoa jana yake kwa sababu kila siku anamuona mpya.

“Sijui nieleze nini lakini namshukuru Mungu anazidi kunisimamia katika ndoa yangu na nimekuwa mwenye furaha kila wakati ambapo sasa hivi tayari nimetimiza mwaka lakini namuona Banda kama ndiyo kanioa hivi karibuni, yaani ninampenda sana,” alisema Zabibu Kiba ambaye yeye na mumewe wanaishi Afrika Kusini kwa sasa.


Loading...

Toa comment