The House of Favourite Newspapers

Unashindwaje Kumiliki Ndinga Mpya kwa Tsh 800 tu – Video

0

 

MAMBO si ndo haya sasa, ukiwa mjanja kwa kusoma magazeti ya Championi au Spoti Xtra kila wiki, unaweza ukawa miongoni mwa watu ambao wanaweza wakalala masikini na kuamka matajiri huku ukitia wese na kuendesha ndinga yako mpyaa kwa Tsh 800 au jero tu.

 

Hii ni bahati nasibu ambayo Championi na Spoti Xtra wameamua kumtunuku mtu wake mmoja wa nguvu, katika karne hii ya 21.

 

Ona, yaani unanunua gazeti la Championi kwa shilingi 800 au Spoti Xtra kwa tsh 500, unapata habari kali za Bongo za michezo na burudani, unapata makala tamu za ndani na Ulaya, halafu kama hiyo haitoshi, mwisho wa picha unaondoka na Toyota FunCargo mpya, unaenda kuwatambia  mtaani kwenu.

 

Pengine haujanielewa, Ishu inayokimbiza kwa sasa katika mitaa mingi ya nchi hii, ni bahati nasibu iliyoanzishwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra.

 

Bahati Nasibu hiyo iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya, inawahusu wasomaji wote wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra, ambayo yanazalishwa na Kampuni Mama ya Global Publishers.

 

Lakini mbali na mshindi wa jumla kuchomoka na ndinga, wapo ambao kila wiki watakuwa wanajidai na simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.

Timu ya masoko ya Championi na Spoti Xtra, ikiongozwa na Anthony Adam, imekuwa ikizunguka katika mitaa mbalimbali ya Tanzania, ikiwa inatoa elimu kwa watanzania ambao bado hawajapata uelewa mzuri juu ya bahati nasibu hiyo.

 

Leo Ijumaa, timu hiyo iliendelea na ziara yetu ya kulizunguka jiji la Dar es salaam, katika mitaa ya Mbezi Kwa Msuguri, Mbezi Mwisho na  Goba Njia Panda na kuendelea kuwahamasisha watu kuendelea kusoma magazeti ya Championi na Spoti Xtra na kushiriki bahati nasibu hiyo.

 

Katika maeneo yote kilipopita kikosi hicho walibahatika kununua Championi walizisifia habari zilizoandikwa ikiwemo hadithi za kusisimua, makala za burudani na michezo. Kikosi hicho kitaendelea kuzunguuka viunga mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya kuinadi Bahati Nasibu hiyo.

Akizungumza na www.globalpublishers.co.tz, Mkuu wa Idara ya Maosko na Usambazaji wa global Publishers, Anthony Adam amesema; “Katika kila mtaa tuliopita tuligawa zawadi za bure kwa watu wote ambao walikutwa na gazeti la Spoti Xtra, tulichezesha droo kwa washiriki wote na walijinyakulia zawadi za papo kwa papo.

 

“Kwa wale wa mikoani, zamu yao ya mtaa kwa mtaa inakuja, ambapo wiki ijayo tutanza na mkoa wa Mwanza, kisha tutaenda Arusha, mbeya, Tanga na tutaendelea kuzunguka katika mikoa yote ya Tanzania na gari letu la matangazo, ambapo kutakuwa na wacheza shoo ambao watakuwa wanatoka burudani huku wanaitangaza bahati nasibu yetu.

 

“Kikubwa waendelee kufuatilia magazeti yetu na mitandao yote ya kijamii inayomilikiwa na Global Publishers, kama vile Global Tv Online, +255Global Radio, magazeti yote, Instagram page ya Global Publishers, Global TV Online, +255Global Radio, Facebook na kwenye website zote za Global Publishers, ambako huko tutakuwa tunaweka taarifa zote,” alisema Adam.

Mbali na hilo, Adam aliendelea kuwakumbusha wasomaji wa Spoti Xtra na Championi kuwa, bahati nasibu hiyo ndiyo kwanza imefikisha wiki moja na siku tatu, lakini itakwenda kwa muda wa miezi mitatu, hivyo alitoa wito kwa watu wote kuendelea kushiriki.

 

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, aliwaondoa hofu watanzania kuwa hakuna mtu ambaye amendaliwa ushindi, kwani bahati nasibu hiyo imefuata utaratibu wote na itaendeshwa kwa uhuru na haki ili kupata mshindi anayestahili.

 

Mbali na hilo, Mrisho alisema kuwa wale washindi wa Simu aina ya Smart Kitochi wataanza kutangazwa kuanzia wiki ijayo, ambapo watu 10, wataondoka na simu hizo ambazo zitakuwa zimesheeni bando la bure na App ya Global ambayo ina uondo wote wa kimichezo, kisiasa na Kiburudani.

“Niwaondoe hofu wasomaji wote wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra, hakuna mshindi ambaye amepangwa kuondoka na gari au kushinda simu kila wiki, hii ni bahati nasibu ya kila mtu, yaani hata wewe unayesoma hivi sasa unayonafasi ya kushinda, unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti mara nyingi na uweze kujitengenezea nafasi ya kushinda.

 

“Kumbuka hakuna kikomo cha ushiriki,  kama unaweza kunununua magazeti 10 au 20, wewe nunua na ujaze taarifa zako, unachotakiwa kuzingatia ni kwamba taarifa hizo ziwe za kweli ili isije kuleta shida baadae,” alisema Mrisho.

 

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi au Spoti Xtra, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

 

Leave A Reply